BAADA YA UVUMILIVU KUWASHINDA PADRI NA SISTA WABADILI DINI ILI WAOANE


 
ASKOFU MSAIDIZI WA KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI ELINGANYA SARIA AMEFUNGISHA NDOA YA PADRE NA SISTA BAADA YA WAWILI HAO KUSHINDWA KUVUMILIA MAISHA YA UTUME.

IBADA YA NDOA ILIHUDHURIWA NA MAELFU YA WATU KUTOKA NDANI NA NJE YA WILAYA ROMBO NA NDOA HIYO IMEFANYIKA KATIKA USHIRIKA WA ROMBO MKUU JIMBO LA KILIMANJARO MASHARIKI KWENYE DAYOSISI YA KASKAZINI.

AKIONGEA KATIKA IBADA HIYO YA NDOA  ASKOFU ELINGAYA ALISEMA BW:HARUSI AMBAYE KWA SASA NI MCHUNGAJI BONIFACE SILAYO KABLA YA KUWA KKKT HUKO NYUMA ALIKUWA MWANAFUNZI WA MAFUNZO YA UPADRI WAKATI BI: HARUSI DR:ELIASIFIWE KILEO ALIKUWA MTAWA.

"Bwana harusi alikuwa muumini wa kanisa katoliki,ambaye alikuwa akisomea upadre katika jimbo la Moshi,huku Bibi harusi akiwa tayari ni mtawa wa shirika la Neema mkoani Kilimanjaro.Baada ya kuacha utume wao,Bwana harusi aliamua kujiunga na dhehebu la KKKT akawa katika uangalizi maalumu kabla ya kusomea uchungaji hatimaye kubarikiwa kwa utumishi huo"alisema Askofu Elingaya.

Alisema kabla ya kuwafungisha ndoa hiyo,uongozi ulikaa kwa muda ukiwahoji na kuangalia mienendo yao ambapo walitoa sababu kuwa hawakuwa na wito wa kuwa padre na sister kwani ndoto yao walihitaji kuwa na familia.
 
KWA UPANDE WAKE MKUU WA KKKT JIMBO LA KILIMANJARO MASHARIKI  MCHUNGAJI WILFORD MOSHA AKIELEZA CHANGAMOTO ZA NDO KATIKA JIMBO LAKE ALISEMA FAMILIA NYINGI ZIMESHINDWA KUISHI KUTOKANA NA TATIZO LA ULEVI ULIOKITHIRI LICHA YA JITIHADA KUBWA YA ELIMU YA NDOA INAYOTOLEWA.



CHANZO: GAZETI LA NYAKATI
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment