TOLEO JIPYA LA BIBLIA LENYE MABADILIKO YA MANENO 52 YA KULETA USAWA KIJINSIA LAINGIZWA MITAANI MJADALA MKUBWA WAIBUKA



Mjadala mkali umeibuliwa na kamati ya kutafisiri maandiko ya bibilia duniani crosway baada ya kuyafanyia marekebisho maneno 52 ya kitabu hicho kinyume na wakati dunia iliyomo.

Wasomi nguli wa bibilia na elimu ya kikristo wanasema na elimu ya kikristo wanasema kuwa toleo hilo jipya ni hatari katika kuindeleza injili ya yesu duniani na kwamba maneno yake mapya yanapaswa kupuuzwa.
  
Aidha bodi ya wakurugezi wa shirika hilo wanadai kuwa wazo la mabadiliko hayo lilitolewa na wajumbe wa bodi hiyo mwaka 1998 japo hawakushirikisha wadau mbalimbali.

Shirika la crossway linadai kwamba toleo hilo  jipya la bibilia linaloondoa ubaguzi wa kijinsia litabaki kuwa hivyo bila kukufanyiwa marekebisho mpaka muda wake wa kisheria utakapomalizika baada ya miakak 17.

Moja ya utata wa mabadiliko hayo upo katika mwanzo 3:16 kwa bibilia ya kawaida katika andiko hilo inasomeka hivi "akamwambia mwanamke hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala" 

Katika toleo hilo jipya linasema "Tamaa yako itaenda sambamba na ya mumeo ila atakutawala"  ikiwa na maana kwamba watatamaniana.

Profesa wa Agano jipya katika seminari ya Northern Scot McKnight,alisema kuwa mabadiliko ya neno hilo la mwanzo 3:16 yametoa maana halisi ya andiko husika.
  "Tafsiri hii mpya ya andiko la mwanzo 3:16 inaonesha kwamba laana ya Mungu aliyoitoa kwa mwanamke haikuwa sahihi ilikuwa ni ya chuki dhidi ya mwanamke" alisema Prf McKnight hivi karibuni katika mahojiano maalumu kwenye mtandao wa Christian Post.

Christian Post lilipomuuliza Mcknight  kama anafikiri toleo hilo jipya la Biblia halitakuwa na upinzani duniani,alidai kwamba hategemei upinzani japo kuwa alikiri makosa ya kuichapisha Biblia hiyo bila kuitisha maoni ya wadau mbalimbali.

Tafsiri zingine za Biblia kama The New International Version na Standard Version,zimebadili maneno "man" ikimaanisha mtu lakini wa jinsia ya kiume sasa inakuwa "human being" kwa maana ya mwanadamu bila kuitaja jinsia yake.

Sehemu zenye neno "brethren" kwa maana ya ndugu limewekwa "brothers and sisters" lengo likiwa ni kuweka usawa wa kijinsia katika maandiko.

Mabadiliko mengine yaliyofanyiwa mabadiliko ni katika Wafalme 1 8:48,Waefeso 1:5 na Yakobo 2:10.
 
Profesa Carolyn Custis James,aliyebobea katika masuala ya Biblia katika seminari ya Theolojia ya Hatfield-Pennyslvania Marekani amesema katika uchunguzi alioufanya muda mchache baada ya toleo hilo kuingia mitaani,amegundua kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa wa wachungaji juu ya mabadiliko hayo.

Hata hivyo anadai kwamba yeye mwenyewe binafsi anaunga mkono mabadiliko hayo akidai kuwa yataimarisha usawa wa kijinsia katika kazi ya Mungu na Neno lake tofauti na sasa. 




Chanzo: Gazeti la Nyakati
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment