ASKOFU BATENZI AZINDUA PARISH MPYA MKOANI MWANZA


Wakristo wametakiwa kupenda mafundisho ya neno la Mungu ili kuepukana na uzushi unao enezwa na baadhi ya watu juu ya injili ili waweze kufika katika ufalme wa mbingu. 

 

Hayo yamesemwa na askofu mkuu wa kanisa la Free Pendekoste Church of Tanzania(FPCT)Askofu David Batenzi,alipokuwa anazindua parishi mpya ya Mhonze mkoani Mwanza.

Amesema kuwa maombi na mafundisho ni nguzo imara kwa mkristo ndiyo maana Yesu alifundisha watu kwa njia ya maombi.
 
Askofu Batenzi  pia amewaasa waumini wa parishi hiyo mpya  ya Mhonze  kuweka watumishi  walio jawa na roho mtakatifu  ili kuweza kunena kwa lugha mpya na hivyo kujenga mshikamano na umoja katika kumtumikia Mungu.

Kwa upande wake katibu wa kanisa hilo Bw:Joakimu Makama  amepongeza sana uamzi huo wa  kuzindua kanisa hilo kuwa parishi mpya ambapo itakuwa na matawi ya Mhonze,Igalagala,Igombe,Kayenze na Nyang’wilolelwa.
 
 

Aidha Bwana Makama amesema uzinduzi wa kanisa hilo itawapatia wepesi wa kufanikisha kauli mbiu yao inayosema kuwa ‘Leta mamilioni ya watu kwa Yesu’ kupitia mikutano ya injili na ibaada ya nyumba kwa nyumba.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment