BIBLIQURAN YACHAPISHWA NI BIBLIA NA QURAN SASA KUWA KITABU KIMOJA,NDIO MWONGOZO WA DINI MOJA YA DUNIA NZIMAMiaka michache baada ya kuzinduliwa kwa hekalu moja la dini mseto kule Ujerumani linalojulikana kama CHRISLAM,likikusanya dini zote chini ya paa moja,dunia imestaajabu tukio lingine muhimu kuelekea kutimia kwa unabii wa Yohana(Ufunuo 13),baada ya wasomi wawili kuchapicha kitabu kimoja kinachojumuisha vitabu 66 vinavyounda Biblia na aya zote zinazounda Quran ili kuchukua nafasi ya Biblia na Quran zinazotumika kwa sasa.


Wasomi hao Safi Kaskas na Dk.David Hungerford waliobobea katika tafsiri ya Quran na Biblia,wanadai kuwa kitabu hicho kinachokusanya kwa pamoja maudhui ya Biblia na yale ya Quran,kitakuwa daraja muhimu kufikia umoja wa kidini,utakaowafanya wanadamu kumwelewa Mungu vyema na hivyo kusali pamoja bila kusigana kama ilivyo sasa. 

Wawili hawa pia wanatajwa kuwa ni werevu katika kutafsiri vitabu vya dini za Kiislamu na Kikristo,kwa kujibu maswali magumu yanayohusu misimamo ya imani na pia ni wajumbe katika baraza la Kufikia Umoja wa Kidini liitwalo Bridges to Common Ground.

Wanasema kuwa lengo lao kuu ni kuudhihirishia ulimwengu kuwa kitabu cha mwongozo wa dini ya kiislamu Quran,hakiungi mkono waumini wa dini hiyo kuua watu wa imani nyingine kwa jina la Mungu wao “Allah”lakini kinawahimiza kutafta njia ya kuishi na wale wasio Waislamu kwa amani na umoja.  

 
Wakinukuu Quran 5:48,wanasema kuwa kitabu hicho kinaonesha kuwa Mungu aliumba makundi ya watu katika tofauti za kidini na alitaka waishi hivyo na kama angetaka,angewaumba na utashi wa kuamini dini moja tu.Wataalamu hao wanasisitiza kuwa zipo sura nyingi katika Biblia na Quran zinazoeleza kwa pamoja kuwa Mungu ni wa huruma wakitoleaa mfano wa Zaburi 145:8


Kulingana na taarifa ya mtandao wa Christian  Post,wasomi hao wawili wanatimiza unabii kwa kulainisha misingi yenye kukinzana baina ya Uislamu na Ukristo na kuweka njia sawa kufikia hatma ya dunia hii ya kuwa chini ya mtawala mmoja, dini moja na serikali moja ya dunia na kwamba jukumu walilopewa wametimiza kwa mafanikio makubwa.

Nani amewatuma kufanya kazi hiyo na wanafanya kwa maslahi ya nani?Hayo ni maswali yaliyoibuliwa na wasomi wapinzani baada tu ya kutolewa hadharani kwa kitabu kipya mbadala wa Qurani na Biblia zinazotumika kwa sasa.

Profesa Leonardo Maniford mmoja wa wachambuzi wa matukio ya mwenendo wa dunia,anaelezea kazi hiyo kama hatua ya juu kabisa ya makundi ya waandaaji wa mfumo mpya wa dunia,wa kuingiza sayari hii katika mkataba wa kumwabudu Lusifa(Shetani)kwa siri kubwa.

Inaelezwa kuwa kitabu hiki kinaandaliwa kama mwongozo wa ukamilishwaji wa kazi ya ChriSlam,ili kuipitisha kwa siri katika mabaraza ya makanisa na kupata msimamo mmoja kabla ya kukabidhiwa Umoja wa Mataifa katika kile kinachoonekana kuwa ni kujenga umoja wa kweli wa kidini na kufutilia mbali vitabu vyenye tafsiri inayounga mkono ugaidi.


 

Chanzo:Gazeti la Nyakati
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment