HISTORIA YAANDIKWA VISIWANI MAFIA VIJANA 3O WAPOKEA KIPAIMARA


 -Mhashamu Eusebius Nzigilwa

Askofu Msaidizi Wa Jimbo Kuu Katoliki Dar Es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa Amekemea Waamini Wanaopenda Kufuatilia Vyombo Vya Habari Vya Kidunia Kuliko Vya Kanisa Na Hivyo Kufanya Kazi Ya Uinjilishaji Kuwa Ngumu.



Hayo Yamesemwa Katika Misa Takatifu Ya Kutoa Sakramenti Ya Kipaimara Katika Parokia Ya Teresia Wa Mtoto Yesu Mafia Ambapo Takribani Vijana 30 Walipokea Sakaramenti Hiyo Idadi Ambayo Haijawahi Kufikiwa Katika Kisiwa Hicho Cha Mafia Chenye Zaidi Ya Asilimia 90 Ya Wakazi Wake Ni Waislamu.



Aidha  Amesema Kuwa Yesu Amewaagiza Watu Waende Ulimwenguni Kote Wakatangaze Injili Hivyo Hawapaswi Kupinga Agizo La Mungu Na Kwamba Atakayemuonea Aibu Naye Atamuonea Aibu Mbele Ya Baba Yake.



Askofu Huyo Amewaasa Vijana Waliopata Sakramenti Ya Kipaimara Kuwa Hata Wao Wanatumwa Kuitangaza Injili Na Kuwataka Waitangaze Huruma Ya Mungu Bila Uwoga Kwani Huu Siyo Wakati Wa Kujificha.


Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment