KIFAHAMU KIKUNDI KIPYA CHA MUZIKI WA INJILI KINACHOITWA MJ BAND


Kutoka studio za 98.2 Kwaneema Fm Radio za jijini Mwanza Tanzania,Mwanadada chipukizi kabisa mwenye sauti ya kuvutia Joyce Kuzenza ametambulisha wimbo wake unaokwenda kwa jina la "NAKAZA MWENDO"

Joyce ametambulisha wimbo huo kwenye kipindi mahili cha burudani kinachoitwa FULL SHANGWE EXTRA ambapo amesema wimbo huo umetungwa naye mwimbaji mahili wa nyimbo za injili anayeitwa Mlemba mo.

Wimbo huo ambao amemshirikisha mwanadada mwenzake anayeitwa Mariam pamoja naye Mlemba mo,unazungumzia maisha ya kutokata tamaa na kukaza mwendo katika kuzidi kutafta mafanikio ya kimiwli na kiroho.

Aidha kupitia kipindi cha Full shangwe extra,Joyce ametambulisha rasimi kundi jipya la muziki wa injili linaloitwa MJ BAND lenye waimbaji wawili tu ambaye ni yeye mwenyewe pamoja na mwenzake Mariam waliyeshirikiana kwenye wimbo huo.

-Sikiliza hapa chini mahojiano yao MJ BAND kwenye kipindi cha full shangwe extra.


 -Kutoka kushoto ni Joyce Kuzenza pamoja na Mariam wanaounda MJ BAND
MJ BAND ni kikundi kipya cha muziki wa injili kutoka jijini mwanza ambao wataendelea kutoa kazi nzuri kwa pamoja.Wako chini ya usimamizi wa PROMOVER MANEGEMENT na iwapo utawahitaji kwa ajili ya mialiko mbalimbali au masuala yoyote ya kimuziki,tafadhali wasiliana na uongozi kwa simu namba 0784 074 462.

-Download/Sikiliza hapa chini wimbo wa Nakaza Mwendo. 
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment