MTOTO WA ROSE MUHANDO ATOA VIDEO NYINGINE,AMESHIRIKIANA NA MMAREKANI ITAZAME HAPA


Annoint Essau Amani maarufu kwa jina la mtoto wa Rose Muhando,ameendelea kufanya vizuri katika tasnia ya uimbaji wa nyimbo za injili baada ya kutoa video ya wimbo mpya alioshirikiana na mtanzania anayeishi nchini Marekani anayeitwa Fidel Murua.

Wimbo unaitwa UJE LEO ni wimbo ambao Amani ameshirikiswa na mtanzania Fidel Murua unaozungumzia jinsi maisha yanavyozidi kugubikwa na changamoto za kidunia huku baadhi wakishindwa kuzikabili.

Akizungumza na PROMOVER.COM Amani anasema wimbo huo una ubunifu mkubwa kwani pamoja na kwamba katika audio na video yeye na Fidel wanaoneka wakiimba kwa pamoja ila ukweli ni kwamba wamerekodi wakiwa mbalimbali yaani mmoja akiwa Tanzania na mwingine akiwa Marekani,hivyo kukua kwa teknolojia kumefanikisha jambo hilo gumu kuwa jepesi.

Audio imetengenezwa na Producer Nas b ndani ya studio ya Pamoja Records huku video ikiwa imetengenezwa nchini Kenya naye direcror CryStal kutoka studio ya CryStal Media lab.

-Itazame hapa video hiyo
Annoint Essau Amani hivi karibuni ametwaa tuzo huko nchini Kenya,kufahamu zaidi soma>>HAPA
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment