MWIMBAJI WA NYIMBO ZA DUNIA AKUBALI KUOKOKA BAADA YA KUSHIRIKIANA WIMBO NA MTOTO WA ROSE MUHANDO

 

Baada ya mabishano ya takribani dakika tano,hatimaye Nas B mwimbaji wa muziki wa dunia alikubali kuokoka na kumwimbia Bwana nyimbo za Gospel,ikiwa ni pamoja na kuwawavuta waimbaji wenzake wa kidunia kumwimbia Mungu.

Hayo yamejiri katika wimbo mpya wa kushirikiana kati yake mwimbaji Nas B akiwa ameshirikishwa naye Annoint Essau Amani ambaye ni mtoto wa malkia wa muziki wa ijili nchini Rose Muhando.

 

Wimbo huo unaitwa "WAPI SAHIHI"na ni mabishano baina ya pende mbili mmoja akimtaka mwenzake aimbe gospel na mwingine akipinga kwa hoja na sababu.Lakini mwishowe Nas b akakiri na kukubali kumtumikia Mungu hivyo kazi ya bwana kutimia kupitia uimbaji.

 


























 




Akizungumza na PROMOVERTZ.COM Essau anasema lengo siyo kushirikiana tu mwimbaji wa dunia bali lengo kuu ni kuwaalika waimbaji hao kugeuka na kumtumikia Mungu.

PROMOVER: Hivi ni sahihi waimbaji wa gospel kushirikiana na wale wa kidunia!! hii si ni kumkosea Mungu?

ESSAU:Sikuimba naye ili kuzungumzia kitu chochote cha kidunia,ningefanya hivyo ningekuwa nakosea ila nimeimba naye ili kumshawishi yeye na wengine kumgeukia Mungu na lengo lilitimia.

PROMOVER: Una matumaini gani juu ya huu wimbo?

ESSAU: Natumaini vijana weeengi waliookoka na wasiokoka duniani,watamrudia Mungu maana Yesu anasema ametuandikia vijana maana vijana tunayo nguvu.

Kwa mawasiliano zaidi jinsi ya kumpata Essau kwaajili ya mialiko na shughuli mbalibali za injili piga simu namba:0755 099 942

-Tazama sasa hiyo video hapa chini. 
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment