MWINJILISTI BENADERTHA MAGUMBA:WAKRISTO WENGI WANATAKA BARAKA ZA MUNGU PASIPO KUJITENGA NA DHAMBI


 -Mwinjilisti Benadertha Magumba
Kuiitii sauti ya Mungu na maagizo yake ikiwa ni pamoja na kuyatumikia mungu hufanya jambo katika maisha ya mkristo na baraka zake humpandishwa katika viwango vya juu kama neno linavyosema uliangalia neno lake na kulitimiza.


Hayo yameelezwa na mwinjilisti Bernadetha Josephat Magumba wa kanisa la Holy Ghost Revival Ministry, lililopo miti ya nyerere jijini Mwanza, katika ibada iliyofanyika kanisani hapo hivi karibuni.
Amesema ili Mungu aweze kufanya jambo katika maisha ya mwamini ni lazima aweze kujua Mungu anataka nini na hapendi mambo gani ambayo ni chukizo kwake na kuongeza kuwa wakristo wengi wamekuwa wakitaka baraka lakini hawajataka kujitenga mbali na dhambi jambo ambalo ni chukizo mbele za Mungu na hakuna baraka inayokuja bila kufanya ushirika na Mungu katika roho na kweli.


Aidha mwinjilisti magumba amewataka wakristo kuacha tabia ya mazoea katika kumuomba mungu huku wengine wakizidi kuendekeza mila za koo zao jambo ambalo halimpi Mungu utukufu na kwa kufanya hivyo ni kuendelea kuitumikia miungu na kumfanya Mungu kuwa kinyume nao.
 -Mwinjilisti Benadertha akiwa na mmewe mchungaji kiongozi wa kanisa la Holly Ghost Revival Ministry Josephat Magumba

Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment