NABII ATABIRI MWISHO WA DUNIA KUFIKA KABLA YA UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI MWAKA HUU.













Myahudi mmoja ambaye amejitambulisha kuwa nabii kutoka nchini Israel,Rabbi Alon Anava ametabiri kuja kwa masihi(Bwana Yesu)mara ya pili kabla ya kumalizika uchaguzi mkuu wa Marekani mwezi wa kumi na moja mwaka huu.


Nabii huyo ambaye pia ni mwalimu na mwanafalsafa maarufu duniani,amesema mojawapo ya dalili ya ujio huo ambo ni ishara ya mwisho wa dunia,kutakuwepo na sheria kali ya kijeshi itakayotangazwa na wagombea uraisi nchini Marekani.


Nabii huyo alisema utabiri huo unalenga kuwaweka sawa wayahudi wote kutoka maeneo mbalimbali duniani kwaajili ya kukusanyika pamoja kumpokea Masihi wao(Yesu Kristo)

 











Myahudi huyo aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu ya kituo kimoja cha redio ya wazee nchini Israel,baada ya kutakiwa kueleza dalili zinazoashiria kurudi kwa Masihi kunyakua watesi wake.


Nabii Anava alivitaja baadhi ya viashiria vitatu vya kutimia kwa kwa unabii wake huo kuwa ni pamoja na kutokea kwa baadhi ya mambo ya kutisha na kuumiza vichwa vya wengi katika maeneo mbalimbali duniani.


Alitaja mojawapo ya dalili hizo kuwa ni kutokea kwa nyota kubwa na ndefu yenye mng’ao mkali na  wakutisha iliyopewa jina la Nabiru,ambayo itadumu kwa muda mrefu na kuichanganya dunia na matokeo yake ni maji kufunika sehemu kubwa ya dunia.


Hata baadhi ya watabiri  duniani wameeleza kutokea kwa nyota hiyo kubwa ambayo inaweza ikaangamiza dunia.
 


Akizungumzia kuhusu kutokea kwa vita vya dunia,alisema kutimia kwa unabii wake kunaambatana na matumizi ya silaha kuwa zitakazotumika ambazo ni za nyuklia.


Alipoulizwa kuhusu uhusiano wa mwisho wa dunia na uchaguzi mkuu wa Marekani,alisema 

“Bila shaka uchaguzi huo una uhusiano mkubwa na utabiri huo wa mwisho wa dunia shetani yuko mlangoni ananyatia hivyo wahusika wote wa serikali wanapaswa kulitambua hilo na kusoma alama za nyakati”.

 
 

Utabiri wa Nabii huyo umeungwa mkono na  wayahudi wengine ambao wameanza kuutangaza na kuufundisha huku wakiueleza kwamba umejaa mambo muhimu yaliyotabiriwa japo kuna mambo mengine yaliyotajwa yanaweza kubadilika. 




Chanzo:Gazeti la Jibu la Maisha
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 maoni:

  1. Enter your comment...jaman wapendwa katka bwana nawasihi kumsikilza nungu kuliko kutumia akili yako mwenyewe mwili hupotosha Mungu hawezi ingiza mawazo ya kipumbavu ndan ya moyo Wa mwanadamu hivyo shetan hutumia nafac anayopata kupitia tamaa za mwili wako hvyo kama umepata neno na unadai kuwa umeoneshwa na mungu basi funga na kuomba ukimwuliza mungu je hii sauti yatoka kwako na syo kila unachofkilia unalopoka tu hukumu ya mungu ijuu yako upitoshae ulimwengu

    ReplyDelete
  2. Acha tuone mambo yanavyoenda

    ReplyDelete
  3. Acha tuone mambo yanavyoenda

    ReplyDelete