NENO LA SIKU:NGUVU ZA MAAGANO YA KIPEPO ZINAWATESA WENGI BILA HATIA.

Wakristo wengi wamekuwa wakiishi pasipo kufanikiwa kiroho na kimwili kutokana na nguvu za maagano ya nguvu za giza ambayo yaliwekwa na mababu zao hivyo kuendelea kutesa uzao wote.


Hayo yamesemwa na askofu mkuu wa kanisa la Holly Ghost Revival Ministry Josephat Robert Magumba,wakati wa semina ya siku tatu ya kuvunja nguvu za maagano iliyofanyika katika kanisa hilo lililopo igoma jijini Mwanza.


Akinukuu katika kitabu cha mwanzo 15:8-17 pamoja na kile cha kutoka 20:5-6 Askofu Magumba amesema familia nyingi zimekuwa zikiishi pasipo mafanikio kutokana na laana zilizowekwa na mababu zao ambao waliweka maagano ya kutumikia nguvu za giza ikiwa ni sambamba na sadaka za damu. 

 
Kwa upande mwingine askofu Magumba amesema zipo njia zinazoweza kuvunja maagano hayo ikiwemo ile ya kutafta mafundisho imara ya kiroho ili kuvunja mikataba ya kipepo kwa kumpokea yesu kristo na kumruhusu kuweka agano la roho mtakatifu.

 
Wakizungumza na PROMOVERTZ.COM baadhi ya waumini waliojitokeza katika semina hiyo wamesema wamejifunza vitu vikubwa ambavyo hawakuvijua kabla ambapo wameahidi kuwa mabalozi wa kusambaza elimu ya kuvunja nguvu za maagano.

-Msikilize hapa chini Askofu Magumba Akielezea Nguvu za Maagano:
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment