POLYCARP KARDINALI PENGO ATUMA WATOTO 800 VISIWA VYA MAFIA WAKAHUBIRI INJILI



  
Askofu Mkuu Wa Jimbo Kuu Katoliki Dar Es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Amewaomba Watoto Wa Jimbo Lake Waende Mafia Wakahubiri Injili Ili Watu Wapate Kuokoka.


Akofu Pengo Ameyasema Hayo Wakati Akiwaaga Watoto Jimbo Kuu La Dar Es Salaam Ifakara Na Mpanda Katika Viwanja Vya Msimbazi Centre Jijini Dar Es Salaam Kabla Ya Kuanza Safari Ya Kuelekea Mafia.



Safari Hiyo Imeanza Saa 1:42 Asubuhi Ikiongozwa Na Askari Wa Usalama Barabarani Huku Takribani Watoto 800 Wakiwa Wenye Furaha Wakiimba Na Kusali  Na Hatimaye Waliwasili Mafia Saa 11:30 Jioni.

 
   
Watoto Hao Wamepokelewa Na Askofu Msaidizi Wa Jimbo Kuu Katoliki Dar Es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa Pamoja Na Paroko Wa Parokia Ya Mafia Padri Francis Massawe.


Akiongea Padri Francis Massawe Amesema Kuwa Mafia Ni Kisiwa Ambacho Asilimia 90 Ya Wakazi Wake Ni Waislamu Hivyo Kina Changamoto Kubwa Katika Uinjilishaji Huku Akimuomba Kardinali Pengo Azidi Kuhamasisha Vyama Vingine Vya Kitume Kwenda Kisiwani Humo Kuinjilisha.



Kutokana Na Sensa Ya Watu Na Makazi Ya Mwaka 2013 Idadi Ya Wakristo Kisiwani Humo Ni 1693 Ila Hija Ya Utoto Mtakatifu Kila Mwaka Imepelekea Waislamu 10 Kukubali Kumpokea Kristo Kwa Kubatizwa.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment