SHERIA YA KUBADILI JINSIA YAPITISHWA NCHINI NORWAY,ZAIDI YA RAIA 250 WAOMBA KUBADILI JINSIA


 

Bunge la Norway limepitisha rasmi sheria inayoruhusu watoto wenye umri wa miaka sita na kuendelea kubadili jinsia zao na kuifanya kuwa nchi ya tano duniani kuruhusu sheria hiyo.

Kupitishwa kwa sheria hiyo kunatoa kibali kwa raia wa taifa hilo kubadili maungo tangu wakiwa watoto wenye umri wa miaka sita kwa kutakiwa kujaza fomu maalumu kupitia mtandao bila kufanyiwa oparesheni wala ushauri wa daktari.

sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la Norway juni mwaka huu inaifanya nchi hiyo kuwa ya tano duniani kuwaruhusu watoto kubadili jinsia zao baada ya Malta.

 

Aidha wakati wazazi nchini malta wakitaka uthibitisho wa kimahakama kuhusu uhalali wa suala hilo nchini Norway watoto wanashughulikia wenyewe wakitumia utaratibu huo huo kama watu wazima.

Inadaiwa kuwa wapiga kampeni wa masuala ya kubadili jinsia nchini humo wameungana mkono sheria hiyo mpya huku wataalamu wakitoa angalizo dhidi ya kuungwa mkono huko kwamba kutaleta  madhara makubwa kwa watoto hao watakapokuwa watu wazima.

Sheria hiyo itamtaka mtu  yeyote anayetaka kubainisha jinsia anayotaka ambayo haifanani na ile aliyoumbiwa na mungu,kujaza fomu hiyo kupitia mtandao na kuirejesha huku akiwa ameweka wazi maamuzi yake.

ikiwa mhusika amekamilisha mchakato mzima wa kutaka kubadili jinsia au maungo yake itamlazimu kupata namba ya kitambulisho kipya cha uraia itakayomruhusu kufanya marekebisho katika hati yake ya kusafiria,lesseni ya gari,cheti cha kuzaliwa kadi za benki na fomu nyingingine za utambulisho.
 

Inadaiwa kuwa hadi sasa zaidi ya raia wa norway 250 wameshapeleka maombi yao kwa ajili ya kubadili maungo yao na kisha kubarikiwa na serikali ya nchi hiyo.

"Nimekutana na vijana kadha wa kadha ambapo wananiambia kwamba sheria hiyo imefanywa kuwa nyepesi zaidi  wengine wamejiondoa kutoka  kwenye eneo hili la gaza" alisema wazri wa afya nchini humo Benti Hoie

Aliongeza kuwa watunga sheria walililfikia hilo kwamba linahitaji kiasi fulani cha muda kati ya maombi na sheria hii ya mabadaliko ili kuangalia matokeo  lakini walilitupilia mbali wazo hilo.

Sheria hiyo inamtaka mtu ayetaka kubadili jinsia zake kwanza kupatiwa matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kubadili homoni zake na jaribio la kufanyiwa upasuaji wa jinsia kabla ya kuruhusiwa  rasmi kubadli maungo yake.


Kwa mujibu wa taarifa zaidi kutoka nchini humo taasisi inayohusika na masuala ya jinsia ya Norwegian Association For Gender And Sexual Diversity,ndiyo iliyopunguza umri wa nchi hiyo kufanyiwa upasuaji wa kubadili maungo yao kutokana na miaka saba hadi sita  ya sasa.

Taasisi hiyo inadai kuwa watototo wanatakiwa kuanza na mabadiliko hayo ya kubadili jinsia zao wakiwa bado kwenye ngazi ya madarasa ya chini na siyo ya kati.

Baadhi ya raia nchini humo wanasema Raia yeyote nchini humo anaweza kufanya maamzi ya kugeuza maungo yake ya uzazi na siyo kuangalia umri.

Raisi wa kituo cha benjamini kinachohusika na masuala ya jinsia na kutoa matibabu kwa wale wanaofanyiwa upasuaji wa kubadili maungo yao Mikael Scott aliendelea kupigilia msumari sheria hiyo kwa kutaka baadhi ya  mambo kufanyiwa kazi kwanza.

Alisema ni imani yake kwamba Norway itafuata taaratibu za utoaji ushauri kwa watu wanaotaka kubadili jinsia zao.

Makundi mengine yaliyoonyesha kupinga hatua  iliyofanywa na bunge la nchi hiyo kupitisha sheria ya kuruhusu raia wake kubadili jinsia zao kinyume cha mapenzi ya mungu,yaliitaka serikali ya nchi hiyo kufikiria upya.
"Tuna wasiwasi kuhusu uelewa wa wanasayansi kuhusu hili inamaanisha nini kwa watoto kupandikizwa jinsia  zingine!kuna upungufu wa utafiti zaidi kuhusu hili kwa nguvu zote tunahisi kuwapo kwa tahadhari juu ya hili".Ni matamko ya baadhi ya makundi ya watu nchini humo wakionesha kutounga mkono hatu hiyo.
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment