UZINDUZI WA VIDEO ALBUM YAKE MWASASUMBE UMEIVA,NI JUMAPILI HII YA 23/10/2016

Kama upo jijini Mwanza na mikoa ya pembezoni mwake basi hii si ya kukosa,unachotakiwa kukikumbuka tu ni tarehe 23/10/2016 siku ya jumapili katika uwanja wa ccm kirumba kuanzia saa nane kamili mchana.

Ni katika uzinduzi wa video album yake mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Mwanza anayeitwa Emmnuel Mwasasumbe inayoitwa "Waleti ya Yesu".

Ratiba inaanzia siku ya jumamosi ambapo album hiyo itawekewa mkono wa baraka katika kanisa la EAGT CITY CENTER kwa Mchungaji Michael Kulola,kisha siku ya jumapili ndio utakuwa uzinduzi rasmi kwenye uwanja wa ccm kirumba.Hakuna kiingilio ni bure kabisa.

Waimbji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watakuwepo kusindikiza uzinduzi huo.

-Kwa maelezo zaidi na idadi ya waimbaji watakaokuwepo bonyeza>>HAPA

-Kutazama sehemu ya kipande cha video hiyo mpya ya Waleti Ya Yesu bonyeza>>HAPA
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment