BEATRICE MWAIPAJA,ANGEL BENARD,CHRISTINA SHUSHO NA BONNY MWAITEGE WASHINDANISHWA KWENYE TUZO ZA ARIKA MASHARIKIWaimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania Beatrice Mwaipaja,Angel Benard,Christina Shusho naye Bonny Mwaitege,ni miongoni mwa waimbaji wa nyimbo za injili wanaoshindana katika Tuzo za injili Afrika Mashariki zinazoitwa East Africa Gospel Awards(EAGA)

Tuzo hizo zinazoandaliwa nchini Kenya zinajumuisha waimbaji na wadau mbalimbali wa muziki wa ijili kutoka nchi za Afrika Mashariki ambapo utoaji wa tuzo hizo unategemewa kufanyika tarehe 11 DEC nchini Kenya.

Beatrice Mwaipaja anayetamba na wimbo wa Mungu umenihurumia,amechaguliwa kushiriki kwenye vipengele viwili Wimbo bora kuabudu na video bora ya mwaka kwa wimbo wake wa Mungu umenihurumia.

Angel Benard anashindanishwa katika vipengele vinne,Album bora ya mwaka(New Day)Wimbo bora wa mwaka(Salama)Wimbo bora wa kuabudu(Salama) na Wimbo bora wa Rege/Dansi wa mwaka(Need you to reign)


Kwa upande wake Christina Shusho yeye yuko kwenye kipengele kimoja cha Mwimbaji bora wa kike wa mwaka,ambapo anashindana na waimbaji wengine Mercy Masika(Kenya) Tonzi(Rwanda) Janet Otieno(Kenya) Judith Babirye(Uganda) na Gambi Kamanzi(Rwanda).Bonny Mwaitege yeye kachaguliwa kushindana katika kipengele cha Mwimbaji bora wa kiume wa mwaka,ambapo anashindanishwa na waimbaji wengine Kim(Rwanda) Isreal Mbonyi(Rwanda) Pastor Bugembe(Uganda) Bahati(Kenya) na Piston(Kenya)

 
Watanzania wengine waliochaguliwa kushindana kwenye tuzo hizo ni pamoja na Calvary G Band kipengele cha Bandi bora ya mwaka.

Innocent Mujwahuki yeye ni kwatika kipengele cha mzalishaji bora wa muziki(Audio Producer of the year)

Mbagwa Hassan anashindana kwenye kipengele cha mwongozaji bora wa video wa mwaka.

Victoria Martin anashindana kwenye kipengele cha Mlimbwende/Mwanamitindo wa kike wa mwaka.

Kampuni ya Makeke ya nchini Tanzania inashindana katika kipengele cha Nembo bora ya Mitindo ya mwaka.

Jinsi ya kuwapigia kura Washiriki hawa ni rahisi sana.Kuwapigia kura sasa bonyeza>>HAPA 
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment