HONDWA MATHIAS ATIMIZA AHADI YAKE YA KUTOA MISAADA KWA YATIMA NA WAJANE

 

Jana Nov 24 2016 Mwimbaji wa injili kutoka nchini Tanzania Hondwa Mathias,alitimiza ahadi yake ya kutoa misaada kwa yatimba na wajane kupitia tamasha lake lililofanyika hivi karibuni.

Hondwa aliahidi kuwa mapato ya tamAsha hilo yatasaidia watoto yatima na wajane,na kama alivyoahidi amefanya hivyo katika tukio lililofanyika mkoani Mwanza.

Msaada huo ameutoa katika kijiji cha ilalila kata ya shibula nje kidogo ya jiji la Mwanza,ambapo wajane na yatima kutoka kwenye kituo cha kanisa la Pentecoastal Calvary ushindi la kijijini hapo walinufaika na msaaada huo.

Akizungumza na PROMOVER.COM hondwa amesema hataishia hapo bali ataendelea kutoa msaada kwa makundi maalumu kadri anavyopata,ambapo amewataka watanzania kujenga tabia ya kuwasaidia wahitaji kwani kwa kufanya hivyo ni  kujiwekea hadhina mbinguni na wala si kupoteza.

Msaada uliotolewa ni pamoja na Mahindi,sabuni,vitenge,madaftari na kalamu,sare za shule.

Karibu sasa utazame picha za tukio zima la hafla hiyo 
 
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment