JE!NI KWELI SOUL BROTHERS WAMETENGANA? MAJIBU SAHIHI YAKO HAPA

Kumekuwepo na maneno mengi baada ya ukimya wa muda mrefu wa kikundi cha waimbaji wa nyimbo za injili cha jijini Mwanza kinnachoitwa Soul Brothers,wengine wanasema kikundi hicho kimevunjika na kila mtu anafanyakazi kivyake huku wengine wakisema wametengana na meneja wao.

Ukweli kuhusu sitofahamu hiyo umewekwa bayana na msemaji wa kikundi hicho Musa Isaya ambaye pia ni mwimbaji wa kikundi hicho wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Full Shangwe Extra cha kituo cha redio 98.2 Kwaneema fm redio cha jijini Mwanza.
 Yohana Mwachali

 -Musa Isaya
Musa amesema ukimya wao umesababishwa na mambo ya ndani ya kiutendaji ambapo meneja wao alikuwa akishughulikia suala la wao kuendelea au kutoendelea kurekodi katika studio moja tu.

Kuhusu kutengana Musa amesema tarifa hizo ni za uongo kwani bado wako pamoja na kwa sasa wanashighulikia suala la kurekodi video ambalo liko katika hatua nzuri. 

-Sikiliza hapa chini maelezo zaidi wakati wa mahojiano hayo 

-Download/sikiliza wimbo wao soul brothers unaoitwa Uwe wangu Bwana
-Kukifahamu kwa undani kikundi hicho na Kusikiliza wimbo wao mwingine unaoitwa Nakusubiri,bonyeza HAPA
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment