KWANEEMA FM RADIO YAMALIZA BIFU KATI YA CHRISTIAN KELVIN NA MOSES SIMKOKO

 Kushoto ni Moses Simkoko akiwa katika studio za Kwaneema fm radio
Ni bifu iliyoanzia kwenye mtandao wa kijamiii maarufu wa what's up baada ya wawili hao kuhitilafiana kutokana na mashairi ya nyimbo zao kufanana sana kwenye idea na hata hata baadhi ya maneno.

Moses Simkoko kutoka Mbeya anasema alishangaa sana baada ya kuona wimbo wenye kufanana sana na wake na hiyo ilikuwa ni baada ya yeye kupost wimbo wake kwenye group la wasap ndipo mwanagroup mmoja akatuma wimbo mwingine unaofanana sana na wake ndipo zilipofanyika jitihada za kumtafta na kumuunga kwenye group hilo mwenye wimbo huo ambaye ni Christian Kelvin.

Mgogoro na bifu hiyo ilianzia rasmi hapo Baada ya Christian Kelvin mwimbaji maarufu kutoka jijini Mwanza kuwekwa kwenye group hilo ambapo Christian anadai alipokea matusi mengi sana inbox kutoka kwa moses baada ya wawili hao kupishana kauli.

Akihojiwa katika kipindi cha full shangwe extra kinachorushwa na kituo cha redio ya kikristo cha jijini Mwanza kinachoitwa Kwaneema fm radio,Simkoko amekiri ni kweli walipishana kauli na Christian hiyo ikitokana na mapokeo ya taarifa.
 Kushoto ni Moses Simkoko akiwa na Mtangazaji Erick Audax
Taarifa nzuri ni kwamba pamoja na kuwa wawili hao wamekuwa katika mgogoro kwa muda mrefu,kupitia kipindi hicho maarufu cha redio chini yake mtangazaji Erick Audax amewezesha kuwapatanisha na wakaombana msamaha kisha kuahidi kuendelea kulitangaza jina la kristo kwa umoja na upendo.

Bonyeza Play kusikiliza mahojiano hayo:
 Christian Kelvin
 Moses Simkoko

Sikiliza/download hapa nyimbo hizo mbili za waimbaji hao,zilizowapelekea kuhitilafiana kutokana na mashairi yake kufanana,na usiache kutoa maoni yako utwambie je! ni kweli nyimbo hizi zinafanana?   
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment