TAZAMA WIMBO MPYA WAKE LINNET NAFULA KUTOKA KENYA|ASANTE BWANA

Kutoka nchini Kenya anafahamika kwa jina la Linnet Nafula,mwimbaji wa nyimbo za injili kwa lugha ya kiswahili.Leo anatualika kutazama wimbo wake mpya kabisa unaojulikana kama ASANTE BWANA.

Katika wimbo huu Linnet amemshirikisha ChyChy ambapo audio imefanyika kweye studio za Crine Music chini yake producer Ihaji na wakati video ikiwa imeongozwa naye JayMenge wa Calm Media.

Akizungumza na PROMOVER.COM Linnet amesema Asante Bwana ni wimbo wa shukrani unaopatikana kwenye album yake mpya."Nashukuru Mungu kwa uaminifu wake kwangu tangu niokoke hadi sasa.Ameongoza hatua zangu na kutimiza ahadi zake juu ya maisha yangu. Hapa nimefika ni kwa neema yake na sijutii kamwe kuamua kumtumikia".

Karibu sasa utazame wimbo huo,natumaini utabarikiwa na wimbo huo ambao unapendeza kuanzia sauti mavazi na hata rangi ya video.Iwapo utamuhitaji Linnet kwaajili ya mialiko katika huduma mbalimbali za ijili yuko tayari.mtafte kwa mawasiliano haya+254 721 565 620
  
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment