USHIRIKIANO BAINA YA TANZANIA NA ISRAEL WAIVA,MATAIFA TISA YAKUTANA ARUSHA KUFANYA MAOMBI
Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Madhehebu Ya Kikrsto Mkoa Wa Dodoma Askofu Dr Eliah Mauza Amesema Kuwa Tanzania Imefungua Milango Ya Baraka Mbinguni Kwa Kuanzisha Ushirikiano Na Taifa Teule La Israeli.

Askofu Mauza Ameyasema Hayo Alipokuwa Akitoa Shukrani Zake Kwa Waumini Wa Madhehebu Ya Kikristo Yaliyoshiriki Katika Maombi Maalumu Ya Mapatano Kati Ya Nchi Ya Tanzania Ambayo Yalikuwa Na Lengo La Kufungua Milango Ya Kiroho,Kielimu,Na Kiteknolojia Yaliyofanyika Mkoani Arusha Kwa Kushirikisha Nchi Zipatazo Tisa.

Amesema Maombi Hayo Yamefanywa Na Kanisa La Tanzania Wakihudhuria Viongozi Wa Serikali Yameonesha Uungwaji Mkono Wa Tanzania Kwa Taifa La Israeli Jambo Ambalo Ni Mwanzo Wa Baraka Kwa Watanzania Hivyo Wanatakiwa Kuongeza Bidii Katika Kufanya Kazi Na Serikali  Kwa Uaminifu Huku Wakimtumikia Mungu Kiroho.

Kwa Upande Wa Serikali Maombi Hayo Yaliwakilishwa Na Naibu Waziri Ofisi Ya Waziri Mkuu Kazi Na Ajira Antony Mavunde,Ambapo Nchi  Zilizoshiriki Ni Pamoja Na Amerika,AfrikaKusini,Nigeria,Kenya,Zambia,Burundi,Norway,Israel Pamoja Na Tanzania.

Itakumbukwa kwamba Serikali ya Tanzania hivi karibuni imesisitiza nia yake ya kuanzisha ubalozi nchini Israel,kutokana na umuhimu wa ushirikiano wa nchi hiyo na Tanzania katika maendeleo ya kilimo,sayansi na teknolojia.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dk Susan Kolimba (CCM),alisema hayo hivi karibuni bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Malindi,Ally Saleh Ally(CUF)lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Sikonge,Joseph Kakunda (CCM).

Ally katika swali lake la msingi alitaka kufahamu sababu zilizochangia Tanzania kukata uhusiano na Israel,sababu za kurejesha uhusiano huo wa kibalozi na msimamo wa Tanzania katika suala la Uhuru wa Palestina.

Akijibu swali hilo,Dk Kolimba alisema Tanzania ilipopata Uhuru mwaka 1961,ilikuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Israel ambapo nchi hiyo ilikuwa na ubalozi wake jijini Dar es Salaam na Tanzania ilitumia ubalozi wake wa Cairo,Misri kuratibu uhusiano na Israel.

Alisema uhusiano huo uliingia dosari baada ya Jumuiya ya Umoja wa Afrika(OAU)sasa Umoja wa Afrika(AU) kuitenga Israel.Hata hivyo,alisema kuanzia mwaka 1973 mpaka leo, kuna mabadiliko makubwa yametokea katika medani za kimataifa ikiwemo kumalizika kwa vitabaridi,kusambaratika kwa Muungano wa Jamhuri ya Kisoshalisti na Kisovieti.

Mambo mengine yaliyobadili medani za kimataifa ni pamoja na kuangushwa kwa Ukuta wa Berlin na kuungana kwa Ujerumani Mashariki na Magharibi pamoja na kupigwa hatua katika usuluhishi wa mgogoro wa Israel na Palestina.

Alitaja hatua hizo kuwa ni kutiwa saini kwa Mkataba wa Kwanza wa Oslo mwaka 1993,wa Pili mwaka 1995 na kuwepo kwa Mpango wa Amani wa Palestina.

Dk Kolimba alisema mwaka 1995,Tanzania ilichukua hatua ya kwenda na mabadiliko ya dunia na kuamua kuhuisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel,ambapo Israel ina Balozi wake Tanzania, mwenye makazi yake Nairobi,Kenya na Tanzania ina Balozi wake Israel,mwenye makazi yake Cairo,Misri.

Uhusiano huo kwa mujibu wa Dk Kolimba,umeendelea kukua hasa baada ya Tanzania kuwa na Sera mpya ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001,inayosisitiza diplomasia ya uchumi na kwa kutambua hatua kubwa iliyopiga na Israel katika kilimo, sayansi na teknolojia,Serikali imedhamiria kufungua ubalozi mpya Israel.

Pamoja na kufungua ubalozi huo,alisema msimamo wa Tanzania katika kutetea haki za wanyonge duniani,wakiwemo watu wa Palestina,bado uko palepale kama ulivyoachwa na waasisi wa taifa.
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment