KANISA LA TFE KWANEEMA KUFANYA TAMASHA KUBWA LA FUNGA MWAKA


Ni tamasha kubwa na la aina yake kuwahi kufanyika jijini Mwanza,likiwa ni maalumu kwaajili ya kufunga mwaka kwa kumshukuru Mungu kwa zawadi kubwa ya uhai.

Tamasha hilo la kusifu na kuabudu litafanyika jumapili ya tarehe 4/12/2016 kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni kwenye kanisa la TFE Kwaneema chini yake Bishop Augastine Mpemba lililopo kona ya msumbiji Nyasaka jijini Mwanza.

Waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Mwanza watashiriki katika tamasha hilo akiwemo: Angel Benard kutoka,Moses Butoi,Ajuwaye Onesmo,Janet John,Jerusalem Choir bila kuwasahau watoto wa nyumbaji Kwaneema Band na wengine wengi.

Hakuna kiingilio katika tamasha hilo ni bure kabisa,pia chakula cha mchana kitatolewa kwa wote watakaohudhulia.

Hii siyo ya kukosa,Wote Mnakaribishwa!

Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment