MASANJA MKANDAMIZAJI KARUDIA WIMBO WA WALTER CHILAMBO SIACHI,TAZAMA VIDEO HAPA


Wote tunafahamu kuwa yule mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za bongo fleva anayefahamika kwa jina la Walter Chilambo hivi karibuni aliokoka na kuamua kumwimbia Mungu nyimbo za injili,kama hukufahamu taarifa hiyo ikufikie.

Baada tu ya kuamua kuimba gospo Walter Chilambo ameonekana kuwagusa wengi kwa baadhi ya nyimbo zake alizoziachia lakini huu hapa huenda ukawagusa wengi zaidi hata wale waliokuwa mashabiki wake akiwa bado anaimba nyimbo za kudunia.

Ni kwamba Walter Chilambo ameonekana kwenye wimbo mpya wake mchekeshaji maarufu nchini Tanzania ambaye pia ni mwimbaji na mwinjilisti Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji,kwenye wimbo huo Walter kashirikishwa.

Ni kwamba original ya wimbo huo ni kutoka kwa Walter Chilambo aliouimba angali mwanabongo fleva wimbo uliojizolea umaarufu mkubwa akimwimbia mpenzi wake ukiitwa 'Siachi'

Sasa alichokifanya Masanja ni kwamba kaurudia wimbo huo wa Siachi lakini yeye katumia mashairi mengine ambapo anamwimbia mke wake waliyefunga ndoa hivi karibuni anayeitwa Monica na wimbo huu sasa unaitwa Monica.

Karibu sasa utazame wimbo huo hapa chini na kisha utoe maoni yako.Ubarikiwe!

Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment