MWANAMUZIKI AAMUA KUSHEREKEA BIRTHDAY YAKE KWA KULA NA WATOTO WA MITAANI


Ni kawaida sana kwa wengi kusherekea siku zao za kuzaliwa kwa kufanya party kubwa kualika marafiki kukata keki kula na kunywa.

Lakini je!umewahi kuwaza kwamba kwenye siku yako ya kuzaliwa uachane na sherehe na mambo yote hayo kisha uadhimishe kwa kula na watoto wa mtaani? Linaweza kuwa jambo gumu lakini kuna mwanamuziki ambaye amekuwa akifanya hivyo kwa miaka kadhaa sasa.

Mwanamuziki huyo anaitwa Emmanuel Mwasasumbe mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania jijini Mwanza,ambaye kwa mwaka wa pili sasa anasherekea birthday yake kwa kula na watoto wanaoishi katika mazingira magumu maarufu kama watoto wa mtaani.

Ikiwa jana 5/6/2016 ni birhday yake aliamua kwenda mtaani na kukusanya watoto wapatao 15 kisha kula na kunywa  nao mlo wa mchana ambapo pia alitumia nafasi hiyo kufahamu changamoto kadhaa zinazowakabiri watoto hao.



Akizungumza na Promover.com wakati wa mlo huo wa mchana katika vibanda vya mama ntilie vilivyopo maeneo ya buzuruga,Mwasasumbe alisema ameamua kuendelea kusherekea birthday yake kwa mtindo huo kutokana na ukweli kwamba siku hiyo pia ina kumbukumbu nzito ya kuhudhunisha kwani ndiyo siku aliyompoteza mama yake mzazi.

Mwasasumbe anasema ataendelea kufanya hivyo kwa miaka mingine yote ijayo na amepanga kufanya jambo kubwa kwaajili ya watoto wa mitaani kwani Mungu ameshamjalia kupata kiwanja na anategemea kujenga kituo cha kulea watoto yatima.

Aidha ametoa wito kwa jamii kubadili mtazamo juu ya watoto hao kwani sio wote wanaoingia mtaani wameingia kwa mapenzi yao,hivyo basi wawasaidie watoto hao kadri wanavyoweza.


Mwasasumbwe pia hakuacha kutoa wito kwa wote ambao wangependa kumuunga mkono katika hatua hiyo kujitokeza huku pia akiwataka wengine kuiga mfano huo wa kuonesha mapenzi kwa watoto hao na yeye atakuwa tayari kabisa kushirikiana na yeyote atakayefanya hivyo.

Promover Manegement inapenda kutoa salamu za pongezi kwa Emmanuel Mwasasumbe kwa hicho alichokianya lakini pia inatoa rai kwa wananchi wote wenye mapenzi mema waige mfano huo.

Je! birthday yako inakuna! na je unaweza kufanya kama alivyofanya Mwasasumbe? kama jibu lako ni ndio tafadhali wasiliana nasi ili tuungane katika hatua zote bila gharama yoyote.
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment