NEEMA NG'ASHA KUZINDUA ALBUM YAKE YA VIDEO SIKU YAKE YA KUZALIWA

 

Mwimbaji wa muziki wa injili anyeitwa Neema Ng'ashaa anategemea kuzindua album ya video inayoitwa TUNAYE BWANA siku ya jumamosi ya tar 31/12/2016 ambayo pia ndiyo siku yake ya kuzaliwa.

Akizungumza na Promover.com Neema amesema anamshukuru Mungu kwa kufikia hatua hiyo ambapo pia amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika huduma yake ya uimbaji.Kama anavyoeleza hapa chini:


"Napenda kumshukuru Mungu amekuwa mwema sana kwangu,nakumbuka hii audio nimeanza kurekodi 2013 katika mazingira magumu sana lakini namshukuru Mungu sikukata tamaa  niliifanya kwa imani.


Mwaka 2016  nimefanyikiwa kufanya video na director Johson Jimmy(Amigo Johson).Album hii ina nyimbo kama Baba tunakutukuza, Tunae Bwana,Mbele ninaendelea,Nakuabudu Bwana,Matendo yako na we Glorify Your  name.


Namshukuru Mungu amekuwa akiwahudumia watu wake kupitia nyimbo hizi.Album hii itatoka tar 31/12/2016 siku hii ni ya muhimu sana kwangu ni birthday yangu ni siku ambayo ninamshkuru Mungu kwa matendo yake makuu anayonitendea tangu nilipozaliwa mpaka leo nauona wema wake.

Naomba sapoti yenu kubwa wadau wote wa muziki wa Injili ndani na nje ya Tanzania ili album hii izidi kufanyika baraka kwa watu wengi jina la Yesu liinuliwe na injili isonge mbele.

Baadhi ya nyimbo hizi zimo you tube kama  Tunae Bwana na Mbele ninaendelea.Niko tayari kwa mialiko pia ukitaka kupata video yangu piga 0673527249".
 
-HII HAPA CHINI NI MOJA KATI YA VIDEO ZAKE NEEMA NG'ASHA
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment