SERIKALI YALIFUNGIA KANISA KWA KOSA LA NABII KULAZIMISHA WAUMINI KUMPA MALI ZAO


Meya Wa Jiji La Mbeya Mchungaji David Mwashilindi Amelifungia Kanisa Kufanya Huduma Za Kiroho Wilayani Humo Kufuatia Tuhuma Kuwa Kiongozi Wake Mkuu Kuwa Amekuwa Akiombea  Watu Na Kuwalazimisha Watoe Fedha Jambo  Ambalo Ni Kinyume Na Taratibu  Za Kidini   Na Sheria  Za Usajili Wa Kanisa.

Tukio Hilo Limeibuka Wakati Huu Ambapo Mkoa Wa Mbeya Umetajwa Kuwa Wa Pili Barani Afrika Kwa Kuwa Na Madhehebu Mengi Ya Kikristo Baada Ya Jiji La Lagos Nigeria.

Kufuatia Matukio Hayo Mkuu Wa Wilaya Amefika Katika Kituo Hicho Cha Maombezi Cha Nabii G Jani Na Kumbana Ili Arudishe Vitu Vyote Alivyowachukulia Watu Hao Ambapo Alifanya Hivyo Kisha Huduma Yake Kufungiwa.

Aidha Meya Wa Jiji La Mbeya Mchungaji David Mwashilindi Ambaye Pia Ni Mchungaji Kiongozi Wa Kanisa La Evangelism Assemblies Of God Eagt Amesema  Jiji La Mbeya Lina Makanisa Mia Nne Na Hamsini Na Kwamba Mtaa Wa Sae Pekee Una Madhehebu Tisa  Wakati Mtaa Wa Simike Ukiwa Kinara Wa Vituo Vingi Vya Maombezi.
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment