SIKILIZA USHAURI HUU WA KINA WA NDOA KUTOKA KWAKE MWIMBAJI GIFT MWAMBAKutoka  Burudani za Promover.com leo tunakutambulishia mwimbaji mpya kabisa katika tasnia ya muziki wa injili nchini Tanzania anayetokea mkoani Iringa akifahamika kwa jila la Gift Mwamba.

Burudani ambayo anatuletea Gift Mwamba ni wimbo unaoitwa NDOA unaozungumzia suala la ndoa na changamoto zake na umuhimu wa kumshirikisha Mungu katika kupata mwenza wa maisha.

Akizungumza na Promover.com Mwamba amesema aliamua kuandika wimbo huo kutokana na historia ya kweli ya maisha yake ya mahusiano hivyo kupata wazo la kuimba wimbo huo.

"Mimi Naitwa Gift George Mzariwa Wa Iringa Mafinga Kwasasa Naishi Mbagala,Nasali Kwa Askofu Mwiche Kizuiani.Niliandika Hii Nyimbo Ya Ndoa Kwakuwa Ni Vitu Ambavyo Hata Mimi Nimekutana Navyo Nikaona Bora Nifikishe Ujumbe Huu Hata Kwajamii Kwani Niliamini Wapo Wengi Kwenye Ndoa Zao Wanalia Kwani Vijana Wengi Sikuhizi Wamekuwa Wakikurupuka Kuanzisha Mahusiano Bila Ya Kumshilikisha Mungu".

"Unajua Katika Maisha Sio Kila Mwanamke Anafaa Kuwa Mke Na Sio Kila Mwanaume Anafaa Kuwa Mume,Mke Mwema Na Mume Mwema Hutoka Kwa Mungu.Kwahiyo Kabla Ya Kijana Kufanya Maamuzi Yoyote Kupata Mke Au Mume Muombe Kwanza Mungu Usipo Fanya hivyo Utakuja Kujutia"Anasema Mwamba.

Wimbo huo umerekodiwa kwenye studio za Sireous Studio chini ya mikono ya Producer D Dammy.Gift Mwamba yuko tayari kabisa kwaajili ya mialiko mbalimbali ya injili kama utamuhutaji mtafte kwa simu namba:0714 693 768

Karibu sasa uusikilize wimbo huo wa Ndoa kutoka kwake Gift Mwamba kama alivyotualika tuusikilize:
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment