WAUMINI WAVAMIWA KANISANI NA KUPIGWA BAKORA BAADA YA KUKATAA KUCHEZA NGOMA


Baadhi Ya Wachungaji Na Waumini Wa Makanisa Yalioko Wilayani Geita Wamevamiwa Na Kupigwa Kwa Fimbo,Mikuki Wakiwa Ibaadani Kwa Madai Ya Kutotii Amri Ya Kuwataka Kucheza Ngoma Za Jadi.

Amri Hiyo Ilidaiwa Kutolewa Na Mwenyekiti Wa Kijiji Cha Lubanda,Kilichoko Kata Ya Busanda Elias Mliyamali Kuwata Wasio Tii Agizo Hilo Kuhama Mara Moja Kijijini Hapo.

Akizungumza Mchungaji Wa Kanisa La Evangelical Assemblies Of God Tanzania(Eagt) Elia Antony Amesema Amesikitishwa Na Amri Ya Mwenyekiti Huyo Kuwalazimisha Kufanya Mambo Ambayo Yapo Kinyume Cha Imani Yao.

Mchungaji Antony Amesema Ngoma Za Jadi Zilikuwapo Tangu Awali Na Viongozi Waliopita Wala Hawakufanya Hivyo Kulazimisha Watu Kwa Kuwa Kila Mtu Ana Imani  Yake.


Kwa Upande Wake Askofu Cpct Mkoa Wa Geita Stephano Saguda Amesema Alipozipata Taarifa Hizo Alizifikisha Kwa Mkuu Wa Wilaya  Ambaye Aliahidi Kulifuatilia Jambo Hilo Na Kutoa Waraka Maalum Kwa Mwenyekiti Huyo Wa Kijiji.

Chanzo:Jibu la Maisha
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment