HONDWA MATHIAS AMFUNIKA GOODLUCK GOZBERT KWENYE NANI ZAIDI


Baadhi ya wadau wa muziki wa injili kutoka jijini Mwanza wamemchagua Hondwa Mathias kuwa mwimbaji bora zaidi kuliko mwenzake wa jijini Mwanza Goodluck Gozbert.

Hayo yamejiri kwenye mpambano wa waimbaji yaani Nani Zaidi kwenye kipindi cha 'Ngurumo za waimbaji' kinachorushwa na kituo cha redio kwaneema fm cha jijini Mwanza.

Kwenye mpambano huo wadau wa nyimbo za injili ambao ni wasikilizaji wa kituo hicho cha redio walipata nafasi ya kupiga simu na kuchagua ni mwimbaji gani wanayemkubali zaidi kati ya wawili hao ambapo hadi mwisho wa kura matokeo yalionesha kuwa Hondwa Mathias a.k.a Hondwa Melody alipata kura 20 huku Goodluck Gozbert akipata kura 18 kati ya 38 zilizopigwa.
Wawili hao ambao wote wana uwezo mzuri wa kuimba huku wakikubalika sana wanatokea katika jiji la Mwanza,Hondwa akitamba na wimbo wa ‘Nani kama Mama’ huku Goodluck akitamba na wimbo wa ‘Hao Hao’.

Ubishi wa nani zaidi kati yao umemalizwa kwa matokeo hayo ya kura zilizopigwa na wasikilizaji,lakini kama wewe hujakubaliana na matokeo hayo tafadhali piga kura yako kwenye comments hapo chini kisha tutatoa matokeo ya kura za wasomaji wa mtandao huu wa Promover.com Karibu sana.

Kwa sasa Hondwa Melody anbaye ameibuka mshindi katika mpamabano huo,anatamba na wimbo wake wa ‘Harusi’ aliouachia hivi karibuni,unaweza kuusikiliza hapa chini:
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

  1. Kwa yeyote mwenye maoni juu ya mbambano huo wa waimbaji,tafadhali aweke hapa maoni yake.

    ReplyDelete
  2. KUWEKA MAONI KUPITIA FACEBOOK BONYEZA NENO FACEBOOK COMMENT HAPO JUU

    ReplyDelete