MCHUNGANJI ASHITAKIWA KWA KUMBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA SABA



 
Mchungaji Wa Kanisa La  Free Pentekoste Church Tanzania (Fpct) Tawi La Gezaulole Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro,Emanueli Mwikizu(42) Amefikishwa Katika Mahakama Ya Wilaya Ya Hai Kwa Tuhuma Za Kumbaka Mtoto Wake  Mwenye Umri Wa Miaka 7.

Akisoma Hati Ya Mashtaka Mahakamani Hapo Mbele Ya Hakimu Anayesikiliza Kesi Hiyo, Anold Kirekiano Mwendesha Mashtaka Wa Polisi,Elisha Moleli Amesema Mtuhumiwa Huyo Alitenda Kosa La Kuzini Akijua Kufanya Hivyo Ni Kosa La Jinai.

Amesema Kuwa Mtuhumiwa Huyo Alitenda Kosa Hilo Mnamo Januari 17 Mwaka Huu  Nyumbani Kwake Mtaa Wa Gezaulo Majira Ya Saa 3:30 Asubuhi Kwa Kumwingilia Kwa Nguvu Na Kumsababishia Mtoto Huyo Maumivu Makali Sehemu Zake Za Siri.

Mtuhumiwa Huyo Amekana Shitaka Hilo Ambapo Hakimu Anayesikiliza Kesi Hiyo Amehairisha Hadi Februari 9 Mwaka Huu Itakapotajwa Tena Na Mtuhumiwa Yupo Rumande Baada Ya Kushindwa Masharti Ya Dhamana.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment