R.I.P ANNOINT ESSAU AMANI 1995-2017 | NITAKUMBUKWA NA NINI?

 

R.I.P Annoint Essau Amani 1995-2017 Nitakumbukwa na nini? Hayo ni baadhi ya maneno yalioyandikwa kwenye picha maalum(photo cover)ya wimbo mpya wa kwanza wake Annoint Essau Amani maarufu kama mtoto wa Rose Muhando aliouuachia mapema mwaka huu wa 2017.

Wimbo huo ambao unapatikana kwenye album yake mpya ya 'Fungua Mboni' unaitwa 'Nitakumbukwa na Nini' ukiwa umerekodiwa kwenye studio Pamoja Records kutoka jijini Dar es salaam.

Huenda wewe ukawa ni mmoja kati ya wale walioshituka baada ya kuona cover ya wimbo huo ikiwa na maneno ya R.I.P lakini ukweli ni kwamba Annoint hajafariki bali tu alihitaji attention ya wadau kuweza kufahamu kinachozungumziwa ndani ya wimbo huo. 

Akizungumza na Promover.com Essau amesema lengo la wimbo huo nikuwakumbusha watu kuwa kuna kifo kwa kila nafsi hivyo basi kila mmoja yampasa kutenda memea kulingana na nafasi yake.

'Usijione wewe ndio wewe,usifikiri umefika duniani wote tunapita,kama unapesa wasaidie wenzio,kama una kazi wapatie na wengine.Lazima ujiulize utakumbukwa na nini lakini pia usaidie wengine wapate cha kukumbukwa watakapofariki' amesema Essau.

Karibu sasa uusikilize wimbo huo lakini kama utahitaji kumpata Annoint Essau Amani mtafte kupitia simu namba:+255 755 099 942
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment