MGOGORO KANISA LA EAGT WAZIDI KUFUKUTA,ASKOFU MAHENE ASEMA HAITAMBUI KATIBA MPYA ILIYOPITISHWA



 Askofu John Mahene(Aliyeshika Biblia)
Mvutano Wa Kiuongozi Umeendelea Kuibuka Katika Dhehebu La Eagt Nchini Baada Ya Askofu Mkuu Msaidizi,John Mahene Kuwataka Wachungaji Wa Makanisa Ya Dhehebu Hilo Kutoitambua Katiba Mpya Ya Eagt Iliyopitishwa Hivi Karibuni Mjini Dodoma.

Askofu Mahene Ameyasema Hayo Hii Leo Jijini Mwanza Wakati Akizungumza Na Wanahabari Katika Kanisa La Eagt Bugando.

Amesema Katiba Hiyo Inayozuia Viongozi Wa Dhehebu Hilo Kuwa Na Umri Usiozidi Miaka 70 Imelenga Kukwamisha Utendaji Kazi Wake Baada Ya Mahakama Ya Hakimu Mkazi Mkoani Mwanza Kusimamisha Maamuzi Ya Kutenguliwa Kwake Kutokana Na Kashfa Za Kiuongozi Zinazomkabiri Hadi Kesi Iliyo Mahakamani Itakapotolewa Maamuzi.

Amebainisha Kwamba Hayo Yanafanyika Ili Kumkwamisha Kujua Yanayotendeka Ndani Ya Uongozi Wa Eagt Ikiwemo Ununuzi Wa Magari Takribani 50 Tangu Mwaka 2005 Hadi 2016 Ambayo Hata Hivyo Hajawahi Kuyaona.

Hata Hivyo Askofu Mahene Amezungumzia Chanzo Cha Mgogoro Huo Ndani Ya Dhehebu Hilo La Eagt Nchini Ambapo pia maetoa msimamo wake kuhusu ufisadi huo ndani ya kanisa,msikilize hapo chini.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment