TAZAMA MKASA HUU JINSI ULEMAVU ULIVYOHARIBU MALENGO YA MAMA HUYU,INASIKITISHA SANA.


Kama wahenga walivyosema "Hujafa Hujaumbika" ndivyo unavyoweza kuelezea mkasa wake Bi Hilda Cliphod Mwasakujonga mkazi wa jijini Mwanza nchini Tanzania ambaye amepatwa na ulemavu wa viungo.

Hilda hakuzaliwa na ulemavu wa viungo bali alianza kulemaa taratibu kadri alivyokuwa ambapo pamoja na kuendelea kulemaa viungo vyake lakini bado aliendelea kufanya kazi zake za ujasiliamali kwani alishindwa kabisa kuendelea na shule.

Kibaya kuhusu mkasa huu ni kwamba kwa sasa ulemavu wake umefika sehemu ambayo hawezi tena kukidhi gharama za matibabu na maisha,anaishi na mama yake ambaye amezeeka sana huku pia ndugu zake wakiwa wameshamtenga na kutompa msaada wowote.
Je! nini kilimsibu Bi Hilda?Je ni ulemavu gani unaomsumbua?Majibu yote yako kwenye makala hii fupi hapo chini.Tafadhali sikiliza na ukiguswa tafadhali toa mchango wako msaidie kwa chochote.

-Bonyeza play hapo chini kusikiliza au pia unaweza kudownload mkasa huo katika makala hii fupi
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment