KANISA LA MICC LAZINDULIWA RASMI JIJINI MWANZA,LIMETUMIA ZAIDI YA MILL 450

 

Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG Barnabas Mtokambali amezindua jengo jipya la kanisa la Mwanza International Community Church (MICC)linaloongozwa na Mchungaji Zakayo na Carol Evelyne Nzogere jijini Mwanza ambalo liko chini ya Tanzania Assemblies of God (TAG).
 
Askofu Mkuu Mtokambali amelipongeza kanisa la MICC kwa kuthubutu kufanya mradi mkubwa namna hii kwa imani
 Askofu Mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali
Aidha amewataka wachungaji wengine waige mfano wa MICC na sio kukaa kungojea mzungu flani aje awajengee.
 Askofu Mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali
Askofu Mtokambali ametaja vigezo vya kuzingatia watu wanapojenga kanisa kuwa ni 1. Ubora - liwe na viwango vya ubora na kuzingatia standards(viwango) vya kimataifa.2- Durability-yawe Majengo ya kudumu na3-Liwe jengo lisilopitwa na wakati mapema (design) 4. Accessible-kanisa liwe linafikika.

Akizungumza na blog hii kuhusu uzinduzi huo Mchungaji wa kanisa hilo Zakayo Nzogere amesema "kwakweli tunamshukuru Mungu kwa kututoa kwenye aibu ya kuitwa kanisa la hotelini na sasa tuna jengo letu wenyewe la kuabudia kwa uhuru".

Kuhusu muda ambao kanisa hilo limetumia kujenga kanisa hilo Mchungaji Zakayo Nzogere amesema "Jengo tumeanza kujenga tarehe 23/June/2015 na tulikuwa na pesa taslimu Shilingi 1,700,000/= (milioni 1 laki saba)."Kwa sasa tumekamilisha 80% ya mradi na tumetumia zaidi ya milioni 450 hadi sasa".
 Mchungaji Zakayo Nzogere na Carol Evelyne Nzongere
Mchungaji Nzogere amesema Jengo hilo la kanisa lina uwezo wa kuketi watu 700 huku hivi karibuni wakitarajia kuanza mradi wa kujenga madarasa ya watoto ambayo pia yatatumika kama nursery school siku za wiki.
"Jengo la shule lipo kwenye lenta sasa mwakani tutaanza project ya ujenzi wa wa kituo cha afya". 
 Mchungaji Zakayo Nzogere na Carol Evelyne Nzongere
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Maaskofu mbalimbali na wachungaji wa makanisa jijini Mwanza pamoja na waumini mbalimbali ambao baadhi walijitokeza kushuhudia muujiza huo.Kanisa lipo Nyegezi jijini Mwanza.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Source:mjap inc       
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment