TAZAMA VIDEO MBILI ZA MWIMBAJI SAYUNI MRITA KUTOKA MOROGORO


Kutoka mkoani Morogoro Mwimbaji wa nyimbo za injili anayefahamika kwa jina la Sayuni Mrita anakualika uweze kutazama video zake mbili kwa mara ya kwanza kabisa kupitia Promover.com

Sayuni Mrita anatuletea nyimbo mbili wa kwanza unaitwa 'Sifa kwa Mungu' na mwingine unaitwa 'Nampenda'.Audio zote zimetengenezwa na producer Steven Deffa wa Cha'ngombe Vijana Choir Studio huku video zikiwa zimetengenezwa na director Amani Joseck na Jordan Joseck kutoka Production ya Enzi Films.

Sifa kwa Mungu:"Huu ni wimbo unaozungumzia Jinsi ambavyo Mungu ametutendea mambo mengi maishani mwetu katika shida mbalimbali lakini akatuinua kutoka huko,hivyo yatupasa tumpe sifa" Alisema Sayuni alipozungumza na Promover.com .Utazame wimbo huo hapa chini.


Nampenda Yesu:Huu ni wimbo unaozungumzia Pendo la Yesu Kristo lilivyo kuu sana kwetu lisilo na mfano,hatakaa awepo rafiki mfano wake.Alisema Sayuni alipozungumza na Promover.com. Utazame wimbo huo hapa chini.
Sayuni Mrita ni mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka mkoani Morogoro anaabudu katika kanisa la Caanan Christian Worship Centre(CAG)chini ya bishop Zephaniah Ryoba hadi sasa anayo album moja tu inayoitwa 'NINACHOTAKA' yenye nyimbo tisa zikiwemo hizo mbili.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Sayuni kupitia mawasiliano yauatayo:

-Email:zion2000tz@gmail.com
-Facebook:Sayuni Mrita 
-Whats App:0686815115
-Simu:06555994992

DVD za album hiyo zinapatikana kupitia mawasiliano hayo juu.
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment