WAKAZI WOTE WA SENGEREMA KAENI TAYARI TAMASHA LA PASAKA LINAKUJA NI 17/4/2017

Hii ni kwa wakazi wa Sengerema pamoja na wilaya zote za jirani,Promover Entertainment wanakuletea tamasha kubwa kabisa la Pasaka litakalofanyika wilayani humo Jumatatu ya pasaka 17/4/2017.

Tamasha hili kubwa na la aina yake litaambatana na uzinduzi wa audio album ya 'UZURI WAKO' yake mwimbaji nguli wa nyimbo za injili kutoka wilayani Sengerema anayeitwa Neema Mbozi.

Waimbaji mbalimbali watakuwepo katika tamasha hilo kama vile Lubango kitula kutoka Mwanza,Alfred Kakungi kutoka Kenya,na kutoka sengerema ni Elly Kanogeleki,Tedy Shindika,Yusuph Ng’umba,Elikana Mahalu bila kumsahau afande Echikaka.

Upande wa kwaya ni pamoja na TAG Geita(Jerusalem Tample),AICT Sengerema Choir na Vijana Sengerema Choir.

Tukio zima litafanyika katika ukumbi wa sengerema sekondari kuanzia majira ya saa nane mchana.Kwa kiingilio cha Tsh 2000/= wakubwa na 1000/= watoto.Hakika hii si ya kukosa kaa tayari.


Kwa mawasiliano Zaidi piga simu namba 0767 423 977/0784 423 977/0753 751 779.Wote mnakaribishwa!
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment