CHRISTINA SHUSHO AJITOA KWENYE TUZO ZA GOSPOMEDIA KUWAPA NAFASI WAIMBAJI WAPYA.


Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Christina Shusho ameomba kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Gospo Awards ili kutoa wigo mpana kwa waimbaji wengine ambao pia wameonekana kufanya vyema katika kipindi hiki.

Shusho ambaye alikuwa amechaguliwa katika kipengele cha mwimbaji bora wa kike, wimbo bora wa Mwaka na Video bora ya mwaka ameuambia uongozi wa GospoMedia kuwa hakufanya hivyo kwa nia mbaya bali kutoa nafasi zaidi kwa wadogo zake pia waonekane.

“Nimefanya kwa moyo mweupe kabisa bila hila yoyote,nimeamua kuwapa nafasi wadogo zangu nao waonekane na ninaahidi kuwasapoti kwa kuwapigia pia nitatoa ushirikiano kwa waandaji popote nitakapohitajika” alisema Shusho

Uongozi wa GospoMedia kwa upande wao wamesema kuwa wamepokea kwa ujumbe wa Christina Shusho kwa upande chanya zaidi na kuahidi kufanya nae kazi kwa namna moja au nyingine.

Mwimbaji mwingine ambaye ameomba kujitoa kwenye tuzo hizo ni mwimbaji Milca Kakete ambaye wimbo wake ulichaguliwa katika kipenge cha wimbo bora wa kuabudu.

Tazama hapa chini ujumbe alioundaka Christina Shusho katika ukurasa wake wa Instagram.

Source:GospoMedia
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment