HUDUMA YA LIFE GIVERS INAWALETEA WAKAZI WA MWANZA SEMINA KUBWA KUWAHI KUTOKEA,USIKOSE!

        

Huduma ya Life Givers chini yake mtumishi wa wa Mungu Mch Godfrey Fungo inakuletea semina kubwa kabisa ya Kuinuliwa kiuchumi,uponyaji,ishara na miujiza katika jiji la Mwanza.

Semina hiyo itafanyika kuanzia Tar 9-16/4/2017 kila siku saa 9:00 Alasiri katika ukumbi wa Vijana Social uliopo jirani na viwanja vya furahisha kirumba jijini Mwanza.
.
Mhubiri Baraka John Maina kutoka nchini  Kenya atashirikiana na mchungaji kiongozi Godfrey Fungo katika mafundisho ya kiroho huku waimbaji mbalimbali wakihudumu katika semina hiyo akiwemo Mess Chengula  na Mc Makondeko kutoka jijini Dar es Salaam wakati kutoka jijini Mwanza ni Manonga Classic,Lubango Kitula,Juliety Busagi,Janet John,Happines Mwakyusa na wengine wengi.

Ewe mkazi wa jiji la Mwanza Usikose katika semina hii kwani mtumishi wa Mungu Mess Chengula atafundisha jinsi ya kuwa mjasiliamali wakati ukimtumikia Mungu na jinsi ya kufanya biashara yenye mafanikio kwa muda mfupi.


Njoo ufunguliwe katika vifungo vya umasikini,mateso na maagano yote ya nguvu za giza.Kumbuka hakuna kiingilio ni Bureeee kabisa!Wote mnakaribishwa!
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment