KANISA LAMPATIA TUZO MBILI MTOTO WA ROSE MUHANDO NA KUMTANGAZA KAMA MFALME WA NYIMBO ZA INJILI AFRIKA MASHARIKI



Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania anayeitwa Annoint Essau Aman maarufu kama mtoto wa Rose Muhando,amekabidhiwa tuzo mbili za heshima za kanisa ambalo pia limemtangaza kama mfalme wa nyimbo za injili Afrika Mashariki.

Tuzo hizo mbili amezipokea kwa mpigo kutoka kanisa la House of prayer international church chini yake Bishop Dokta Furaha Mwakabenga kanisa hilo lipo mpakani mwa Zambia na Tanzania kwenye mji wa Tunduma.

Tuzo alizopewa Annoint ni tuzo ya mwandishi bora wa nyimbo za injili Afrika Mashariki 2017 na nyingine ni mwimbaji aliyeshirikiana(collable)na waimbaji wengi wa injili Afrika Mashariki.

Akizungumza na Promover.com Essau alisema anamshukuru Mungu kwa kilichotokea kwani hakuzitegemea tuzo hizo ambapo amewataka watu wote kuendelea kumuunga mkono katika huduma yake ya uimbaji.  

-Tazama hapa chini tukio zima la utoaji wa tuzo hizo. 
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment