LILE TAMASHA BABKUBWA LA PASAKA WILAYANI UKEREWE NDO LINAWADIA NI JUMAPILI HII,USIKOSE!

     
Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya burudani ya injili wilayani ukerewe Promover Enertainment chini ya tovuti ya injili yaPromover.com inakuletea tamasha kubwa kabisa litanalofahamika kama VUKA CONCERT.

Tamasha hili ni maalumu kwaajili ya kuwachangia wajane yatima na wote wanaoishi katika mazingira magumu katika sikukuu ya pasaka ambapo waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Mwanza watakuwepo kumtumikia Mungu kupitia uimbaji.

Waimbaji watakokuwepo ni pamoja Neema Mudosa kutoka nchini Kongo,na kutoka Mwanza ni Manonga Classic,Ajuwaye Onesmo,Mc double D,Prince J Handrick a.k.a Papa Josee pamoja naye Lubango Kitula.Waimbaji wengine wengi pamoja na kwaya kutoka Ukerewe wataimba.

Washereheshaji katika Tamasha hilo ni watangazaji wa vipindi vya gospel kutoka mkoani Mwanza hapa namzungumzia Peter Abdalah pamoja naye Emmy Reid.

Watu wote wa Mungu wataelekea katika viwanja vya Getruda Mongela siku hiyo ya tar 16/4/2017 wewe je?kwanini ukose!! kumbuka ni kwa kiingilio cha Tsh 2,000 kwa wakubwa na Tsh 500 kwa watoto.

Tamasha hili litaanza majira ya saa 8:00 mchana hadi saa 12 jioni.Njoo tuwavushe wajane yatima na wote waishio katika mazingira magumu katika tamasha hili la VUKA CONCERT.Usikoseee!watu wote mnakaribishwa.   

Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment