MADAM FLORA AACHIA WIMBO MPYA JIJINI MWANZA,AELEZEA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA



Mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania anayeitwa Madam Frola ameachia wimbo mpya kabisa unaopatikana kwenye album yake mpya itakayotoka hivi karibuni.

Madam frola ameachia wimbo unaoitwa 'Yesu usipite' katika kipindi cha Maximum Promo kinachorushwa kupitia kituo cha redio cha kwaneema fm cha jijini mwanza.

Wimbo huo umerekodiwa katika studio za Push Up Records za jijini Dar es salaam chini ya mikono ya Producer Innocent Mujwahuki.

Madam Frola amesema wimbo huo ni moja kati ya nyimbo zinazomgusa sana na anaamini kila atakayesikiliza wimbo huo utambariki sana.

Lakini pia ameelezea kuhusu album yake mpya ambayo itakuwa mtaani hivi karibuni ambayo itazinduliwa jijini Mwanza ambapo uzinduzi huo utaenda na tukio muhimu sana ambalo atalitangaza hivi karibuni.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment