PROMOVER MANEGEMENT WANAKULETEA WIMBO MPYA-LUBANGO KITULA | ULIKUWEPO.USIKILIZE HAPA

 
Kwa mara nyingine tena Kutoka jijini Mwanza Nchini Tanzania mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili na anayetamba sana kwa sasa kanda ya ziwa aitwaye Lubango Kitula ameachia wimbo mpya kabisa.

Wimbo huo mpya unaitwa 'ULIKUWEPO' ambao umetengenezwa katika studio za quicksound za jijini Mwanza.

Akitambulisha wimbo huo katika kituo cha redio kwaneema fm cha jijini Mwanza,Erick Audax ambeye ni Afisa Mahusiano wa Promover Manegement ambao ndio wasimamizi wake Lubango,amesema wimbo huo umetengenezwa kwenye kiwango cha hali ya juu huku mwimbaji naye akiwa ameimba kwa kiwango kikubwa sana.

Erick Audax amewataka wanaMwanza na waTanzania kwa ujumla kuusikiliza kwa makini wimbo huo kisha kuusambaza ili kuzidi  kumpa hamasa mwimbaji Lubango Kitula katika huduma hiyo ya uimbaji.

Aidha Erick amesema kuwa siku kadhaa tu baada ya kuutambulisha wimbo huo tayari mwimbaji huyo amepata mialiko mingi ndani na nje ya kanda ya ziwa ambapo mwezi wote wa nne ameshajaza booking hivyo kwa atakayemuitaji ni hadi mwezi wa tano.

Kwa mawasililiano zaidi kumpata mwimbaji Lubango Kitula kwaajili ya mialiko mbalimbali na ushauri mtafte kupitia mawasiliano haya promover160@gmail.com au piga simu:0765967667 -Sikiliza hapo chini wimbo mwingine wake Lubango Kitula-Kidogo dogo
Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment