USIKOSE KONGAMANO HILI LA SIKU TANO JIJINI MWANZA,NI KUTOKA KANISA LA HOLLY GHOST MINISTRY



Kanisa la Holly Ghost Revival Ministry lililopo igoma jijini Mwanza chini yake Askofu Josephat Magumba linawakaribisha watu wote katika kongamano kubwa la neno la Mungu kwaajili ya kufunguliwa katika vifungo vya shetani na kuliombea Taifa.

Kongamano hilo limebema neno kutoka kitabu cha Wakolosai 1:13 'Naye alituokoa katika nguvu za giza akatuingiza katika ufalme wa Mwana wa Pendo lake' 

Kongamano litafanyika kuanzia 23-28/5/2017 kuanzia majira ya saa 8 mchana hadi saa 12 jioni katika viwanja vya cocacola kituo cha Ndama igoma jijini Mwanza.

Walete wagonjwa na wote wanaosumbuliwa na vifungo vya shetani watafunguliwa na kuwekwa huru kabisa kupitia jina la Yesu kristo akiye hai.

Waimbaji mbalimbali watakuwepo kuhudumu katika kongamano hilo akiwemo Lubango kitula,Holly Ghost Choir,Muungano igoma choir,Morning star PEM,Ufunuo CRCT,Yohana Ibeho,Ebenezer Band,Oscar Zeze,Aic Mabatini Choir,Umoja Ndofe na wengine wengi.

Hakuna kiingilio katika kongamano hilo ni bure kabisa,watu wote mnakaribishwa.Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0757961279
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment