SYAMBONGA YESU YA MWASASUMBE YAZIDI KUWAGUSA WENGI,ISIKILIZE HAPA!

Kutoka jijini Mwanza nchini Tanzania mwimbaji wa nyimbo za injili Emmanuel Mwasasumbe anazidi kuchanja mbuga kufuatia wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni unaoitwa Syambonga Yesu.

Wimbo huo aliomshirikisha mwimbaji kutoka kikundi cha Soul Brothers Yohana Mwachali umerekodiwa katika studio ya Brothers Music chini ya mikono ya producer Doncer Master.

Zikiwa zimepita siku chache tu tangu aachie wimbo huo,Mwasasumbe ameonekana kukua kihuduma baada ya kupata mialiko mbalimbali ya huduma ndani nan je ya nchi.

Akizungumza na Promover.com Mwasasumbe amesema kwa sasa  yuko jijini Dar es salaamu Kwenye kanisa la EAGT Sinza akitokea mkoani Dodoma alikokuwa amepiga kambi ya huduma ya uimbaji.Amesema anamshukuru sana Mungu kwa kufungua milango ya huduma na kuahidi kuendelea kuachia nyimbo nzuri Zaidi.

Hapa chini nimekuwekea wimbo huo mpya,tafadhali usikilize kisha usambaze kwa marafiki.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment