HUYU NDIYE MUIMBAJI BORA 2017 KANDA YA ZIWA,AWASHINDA WAIMBAJI WENGINE ZAIDI YA 15


Anafahamika kama Kamodee mali ya Mungu muimbaji wa nyimbo za njili kutoka jijini Mwanza ambaye hivi karibuni mapema mwezi huu ameweza kuibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha kumtafta nyota wa 2017 kanda ya ziwa. 

Tuzo hiyo iliratibiwa na radio ya kikristo inayoitwa Ukombozi fm radio katika Tuzo iliyopewa jina la NYOTA ZILIZOTUFIKIA MWAKA 2017 kinyang'anyiro kilichojumuisha waimbaji wengine zaidi ya 15.

Baada ya zoezi la upigaji wa kura kukamilika kura zilizopigwa na wadau mbalimbali wa muziki wa injili kanda ya ziwa hatimaye Kamodee aliweza kuibuka mshindi katika Tuzo hiyo akipataka jumla ya kura 18,643.

Zoezi la kukabidhiwa Tuzo hiyo ilifanyika katika kanisa la Ukombozi Ministry wamiliki wa redio Ukombozi ya jijini Mwanza nchini Tanzania.

Baada ya kukabidhiwa Tunzo hiyo Kamodee aliwashukuru waandaaji na wapiga kura wote waliomchagua ambapo aliahidi kuendelea kuachia kazi nzuri na za kuvutia,pia alipata nafasi ya kuimba baada ya kukabidhiwa Tuzo.

Kamodee mali ya Mungu ni muimbaji wa nyimbo za injili katika miondoko ya zuku rumba akiwa chini ya usimamizi wa kampuni ya Promover wamiliki wa mtandao huu wa promovertz.com

Hapa chini tumekuwekea moja kati ya wimbo maarufu kutoka kwake kamodee,tafadhali sikiliza kisha sambaza kwa marafiki:
  
 

Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment