WIMBO MPYA WA DIAMOND WAZUA MJADALA MKALI,MCHUNGAJI APANGA KUMSHITAKI

 
Siku moja baada ya muimbaji wa nyimbo za kidunia anayeitwa Diamond Platnumz kuachia wimbo wake mpya unaoitwa 'Hallelujah' mjadala mkali umeibuka.

Mjadala ulioibuka ni kuhusu uhalali wa neno 'Hallelujah' kutumika katika muziki wa kidunia likisifu mambo mengine badala ya kumsifu Mungu kama ambavyo wakristo wamekuwa wakilitumia.

Katika mitandao ya kijamii mjadala kuhusu jambo hilo unashika kasi huku baadhi wakisema msanii huyo ameidhalilisha imani ya kikristo na huku wengine wakisema ameidhalilisha dini yake kwa kuimba neno linaloashiria kuitukuza imani nyingine lakini pia wapo wanaosema hawaoni cha ajabu msanii huyo kulitumia neno hilo.

Katika wimbo huo msanii huyo amelitumia neno hilo katika mlengo wa kusifia mapenzi na mwanamke na wala si mlengo wa kidini,jambo ambalo limeonekana kuwachanganya watu wengi wakiwemo viongozi wa dini.

Mmoja kati ya viongozi wa dini walioonesha kukerwa na jambo hilo ni mchungaji kiongozi wa kanisa la MICC la jijini Mwanza Pst.Zakayo Nzogere ambaye kupitia ukurasa wake wa Facebook ameandika maneno yafuatayo: 
 
Tafadhali tusaidiane kufikisha ujumbe huu...
TUNATAKA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA LINALOJUMUISHA BARAZA LA TEC, CCT NA CPCT LITOE TAMKO DHIDI YA WIMBO WA "DIAMOND" AMBAO AMETUMIA NENO "HALLELUJAH" WAKATI MAUDHUI YA WIMBO WAKE HAYAENDANI NA MAADILI YA KIKRISTO. 

MATUMIZI YA NENO HILO KATIKA WIMBO HUU YANAUDHI.
PIA NAOMBA WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AFIKISHIWE UJUMBE HUU. 

PIA TUNAITAKA BASATA IZUIE WIMBO HUU HADI MANENO HAYO YAONDOLEWE. 

CC. Bishop David Batenzi, Bishop Tarcisius Ngalekumtwa, Bishop Alex Malasusa.

Kama ungependa kuona maoni yaliyotolewa baada ya chipisho la mchungaji huyo bonyeza picha hapo chini.

Share on Google Plus

About Prom Over

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment