TABORA WAZINDUA TIMU MAALUM YA KUSIFU NA KUABUDU,MAMIA WAJITOKEZA KWENYE UZINDUZI

 
Baada ya kukosekana kwa muda mrefu hatimaye Mkoa wa Tabora umezindua timu maalumu ya kusifu na kuabudu inayojulikana kama Tabora Praise Team(TPT)

Uzinduzi huo ulifanyika juzi kwenye tamasha maalum la kusifu na kuabudu linaloitwa 'Uweponi Mwako Salama Yangu' lililofanyika kwenye ukumbi wa TPSC(Uhaziri)Tabora Campus.
 
TPT ni umoja unaojumuisha waimbaji na wapiga vyombo vya muziki kutoka makanisa mbalimbali mkoani Tabora ambao wamelenga kuwa praise team kubwa na yenye mafanikio kote nchini.

Aidha TPT wanategemea kufanya tamasha lingine kubwa la kusifu na kuabudu litakalokuwa la kufunga na kufungua mwaka na baada ya hapo watakuwa wakifanya matamasha kila mwanzo na mwisho wa mwezi.
 
Kutazama picha zaidi bonyeza>>HAPA
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment