TUNAKULETEA MWIMBAJI ANAYEVUMA KWA KASI KUTOKA TABORA-GIDEON PAUL SIKILIZA WIMBO WAKE HAPA



 
Promovertz.com inakutambulishia kipaji kipya kabisa kutoka mkoani Tabora nchini Tanzania.Huyu ni Mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye anafanya vizuri sana katika huduma hiyo mkoani Tabora na ameendelea kuwagusa wengi kupitia nyimbo zake.


Mwimbaji huyu anaitwa Gideon Paul Magangira mwenyeji wa ambapo Leo tungependa uchukue dakika chache za kusikiliza moja kati ya nyimbo za kijana huyu ambaye hakika ni mahiri katika utunzi na uimbaji.


Wimbo tunaokuletea leo unajulikana kama 'HALLELUJAH' kutoka katika album yake inayoitwa 'Akukumbuke' yenye nyimbo nyingi tu ambazo tutaendelea kuzileta kwako siku hadi siku.


Halelujah ni wimbo wa sifa ukiwa katika mahadhi ya boringo,wimbo umerekodiwa katika studio za Kapstone Production za mkoani Tabora chini ya mikono ya producer Baraka Richard(BK).


Kupitia mtandao huu utaendelea kupata taarifa kumuhusu Gideo Paul,kwa leo hebu sikiliza wibo huo na kama una maoni tuandikie hapo chini pia waweza kuusambaza wimbo huo kwa marafiki zako.Kwa mawasiliano zaidi mpigie Gidion Paul kwa simu namba:0762 700762 au 0686 183714

Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment