HIZI NDO VIDEO ZINAZOTAKIWA,HEBU TAZAMA VIDEO HII MPYA YA MLEMBA MO | TUMESIMAMA

 
Hakika mapinduzi yameendelea kuonekana kwenye muziki wa injili baada ya waimbaji kuendelea kufanya video zenye ubora wa hali ya juu.

Mmoja kati ya waimbaji ambaye ameamua kuingia gharama kubwa katika video ni Mlemba Moses maarufu kama Mlemba Mo ambaye ameachia video yake ya kwanza yenye viwango vya juu.

Mlemba Mo ameachia video ya wimbo wa 'Tumesimama' unaopatikana katika album yake mpya ya 'Wale Wale' aliyoizindua mwishoni mwa mwaka 2017 jijini Mwanza.

Video hii imeongozwa na director Bony Albert wa Perfect Light Studio na hakika ni video bora kabisa ya kufungua mwaka lakini pia ukiwa mwanzo mzuri kwa mwimbaji huyo anayefanya vizuri sana kwa sasa jijini Mwanza kupitia album yake mpya.

Akizungumza na Promovertz.com Mlemba Mo amesema video hiyo ni mwanzo wa kuachia video nyingine zenye ubora kutoka album yake ya 'wale wale' ambapo ameahidi kuachia video nyingine hivi karibuni.

Karibu sasa utazame video hiyo na bila shaka utakubi kuwa ni video yenye ubora wa juu. Kwa mawasiliano zaidi unaweza kumpata Mlemba Mo kupitia namba yake ya simu 0745 018 873
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment