PROMOVER MANAGEMENT WANAMTAMBULISHA KWAKO JACKLINE P MOLLEL,SIKILIZA WIMBO WAKE HAPA

"YOU RAISE ME UP"  ni wimbo mpya wake mwimbaji kutoka jijini Mwanza Jackline P.Mollel wimbo ambao umeachiwa rasmi Apl 30 2018.

Wimbo huu umerekodiwa MP Studio ya jijini Mwanza chini ya Producer Ibra Mwasiposya .

Jackline P. Mollel alianzia uimbaji kwenye kwaya (praise team)na sasa ni mwimbaji binafsi wa injili.

Ameanza muziki rasmi kama solo artist mwaka 2017 akiwa chini ya kanisa la Pentekoste worship center Tanzania kwa bishop  Philipo stanslaus jijini Mwanza .

Jack P ni mwimbaji anaesimamiwa kimuziki na label ya  Promover management.
Akizungumzia ujio wa mwimbaji huyo meneja masoko wa Promover  Peter Abdallah amewaomba wadau wa injili kumpokea Kwa kuusikiliza  nyimbo zake,kutoa ushauri  na kumpa mialiko,mwimbaji huyo.  
Jack P ni mwimbaji mwenye familia ya mme na mtoto mmoja,nje  ya Muziki anajishughulisha  na Biashara ndogo ndogo.Kwa mawasiliano mpigie Jack P kwa simu namba:0659926210
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment