Ili kuongeza ufahamu katika mambo mbalimbali hususani mambo ya ujasiliamali na uzalendo wa nchi lazima kila mtu asome vitabu vya kumjenga.
Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa kituo cha redio cha kwa neema fm cha jijini Mwanza Dr:Bishop Augustine Mpemba ambaye pia ndiye askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Field Evangelism(TFE)wakati akizunguza katika hafla ya uzinduzi wa vitabu viwili vya kulipenda taifa na kulijenga na kitabu cha mawazo ya mabilionea.
“Ili mtu yeyote aweze kujikwamua kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ni lazima aongeze maarifa na kutambua wapi alikosea mwanzo na kufuta makosa ya mwanzo bila kukata tamaa na kujifunza jinsi wengine walivyo fanikiwa kwa kusoma vitabu mbalimbali na kuongeza ufahamu”Alisema bishop Augustine Mpemba.
Bi-Shop Mpemba |
Akizungumuzia kitabu cha Kulipenda Taifa na Kulijenga Dr:Bishop Mpemba amesema kuwa kitabu hicho kimekuja katika wakati muafaka ambapo taifa linahitaji viongozi imara,kupiatia kitabu hicho jamii itafahamu jinsi ya kumchagua kiongozi bora wa nchi na kiongozi bora wa yeyote.
“Nchi yetu ina viongozi wa siasa wengi na si viongozi bora,viongozi wa siasa huelekeza nguvu zao katika chaguzi zinazokuja,lakini kiongozi bora huelekeza nguvu katika usitawi wa kizazi kijacho” alisema bishop mpemba na kuiomba jamii kukisoma kitabu hicho ili imutambue kiongozi bora.
Kuhusu kitabu cha Mawazo ya Mabilionea bishop Mpemba alisema kitabu hicho kinafundisha njia bora za namna ya kuwa bilionea na kuondokana na umasikini kwa kuzingatia mambo kazaa.
“tatizo kubwa linalo sumbua jamii ni kuwaza njinsi ya kuanza hatua moja ya ulicho nacho na kukifanya kiwe kikubwa”alisema bishop Mpemba.
Aidha mhasisi yuho wa kituo cha kwa neema fm radio alihitimisha kwa kuiomba jamii imuunge mkono iliaendelee kutoa vitabu vingi na kuendelee kuelimisha jamii hususani elimu ya ujasiliamali na uzalendo wa nchi.
-Kufahamu jinsi ya kuvipata vitabu hivyo,sikiliza maelekezo hapa chini
No comments:
Post a Comment